Sunday, February 26, 2012

UJUMBE KWA WACHUNGAJI

NENO LA LEO:  Yeremia 25:34-35
Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuwawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa. Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka.

TAFAKARI:
Wapendwa! Tunapaswa kujua kuwa tunaishi nyakati za Mwisho na hatari, Yesu alitabiri kuwa wengi hawataokolewa si kwa sababu waliamua hivyo, laa, bali kwa sababu walikoseshwa na viongozi wao wa Dini. Tunashuhudia kila kukicha Wachungaji, Manabii na Mitume wanajitokeza na kuanzisha makanisa, na ujumbe mkubwa ni BARAKA, UTAJIRI, UPONYAJI NA MIUJIZA MINGI. Wachungaji wengi leo ni wachungaji wa MSHAHARA, makanisa ni vitega uchumi sawa na machimbo ya Madini, ndio maana hawana ujasiri wa kukemea uovu. Na wengine bila aibu wanakula Kondoo zao.

Tunashuhudia Wachungaji wengi wakijihusisha na mambo ya aibu kwa SIRI na wengine hata kuanikwa na vyombo vya habari. Pia wengi leo ni wafuasi wa dini za waabudu mashetani na wengine ni free mason, kwa hila wanalaghai watu wengi kwa kujazwa ROHO bandia na Miujiza Mingi – Yesu alisema “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, HATA WALIO WATEULE. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Mathayo 24:24-25, Mathayo 7:21-23.

Wengi wataangamia kwa kukosa MAARIFA (Hosea 4:6), Wapendwa! Miujiza, Kujazwa Roho,Upako, Kunena kwa Lugha n.k. Sio kithibitisho pekee cha Kumtambua mtumishi wa Mungu, kwani SHETANI pia anafanya hayo kwa hila, tunapaswa kujiepusha naye. Siku nyingine nitatoa somo la jinsi ya kuwatambua watumishi wa Mungu na Bandia.

MUNGU WA AMANI AWALINDE NA KUWAPATIA SIKU NJEMA

Ev: Eliezer  Mwangosi
0755808077 & 0652571733
Kwa masomo zaidi fungua mitandao ifuatayo:   http://emwangosi.blogspot.com/ (VIJANA) http://kayanafamilia.blogspot.com/ (NDOA) http://matengenezo.blogspot.com/ (UKWELI HALISI)

MTI USIOZAA MATUNDA

NENO LA TAFAKARI LINATOKA:  LUKA 13:6-9
Akanena Mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na MTINI umepandwa katika Shamba lake la Mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa Shamba la Mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; UUKATE, mbona hata nchi UNAIHARIBU? Akajibu akamwambia, Bwana, UUACHE MWAKA HUU NAO, HATA NIUPALILIE, NIUTILIE SAMADI; nao UKIZAA MATUNDA baadaye VEMA! La, usipozaa, NDIPO UUKATE.

TAFAKARI:
Kati ya matukio ya kusikitisha yaliyotokea katika usiku wa kusherehekea kuvuka mwaka 2011, ni tukio la Baba mmoja aliyefia nyumba ya wageni (Guest House) akiwa na Nyumba Ndogo (Wengine wanaziita VIBANDA HASARA). Kabla ya mauti kumkuta, alisikika akisema “MAADAMU NIMEUONA MWAKA SALAMA! KAZI MOJA ILIYOBAKI NI KULA BATA (KUSTAREHE) KWA KWENDA MBELE” akaanza kunywa kilevi huku akiwa na Kimwana Pembeni. Ilipofika masaa ya alfajiri ndipo wakaenda kumalizia starehe ya Ngono Guest House, taarifa ya mwisho ilikuwa ni yule Baba kukutwa Maiti katika Chumba, Binti akiwa amekimbia na Nyumbani mama na watoto wakisubiri Baba arudi akitokea kwenye mkesha, kwa masikito wakaambulia tarifa za Msiba.

Huyu baba amekufa kifo cha Kipumbavu, kwa sababu badala ya Kumshukuru Mungu kwa kumpatia Uhai tena, yeye akaamua kwenda Kumsaliti Mungu kwa Ulevi na Zinaa. Mungua akaona ni heri apunguze namba ya wanaoharibu shamba lake, matukio mengi kama haya tumeyasikia katika vyombo vya habari. Shukrani zetu anazozikubali Mungu ni kuzaa Matunda Ya Roho Mtakatifu – Soma Wagalatia 5:16-25. Hebu jiulize MALAIKA walishuhudia mambo gani kwako usiku wa kuamkia Mwaka Mpya? Kila mmoja ana majibu yake, na mbinguni yameandikwa kama kumbukumbu za kuletwa siku ya hukuni. Kama ni Ulevi, Ngono nje ya Ndoa halali, na udhalimu wa kila namna, hayo yote yataletwa yakiwa wazi.

Wapendwa hatuko hai leo kwa bahati nasibu, kuna kitu thabiti ambacho Mungu anakitazamia kwetu, mwenye maamuzi ya Mwisho na Uhai wetu ni Mungu, kuna neema ya Yesu Kristo ndiyo inayovuta subira na kututafuta ili tutoke katika maisha ya dhambi, hivyo kusudi la Mungu kutuacha HAI ni ILI TUZAE MATUNDA YA TOBA, au laa kwa wakati tusioutazamia mwenye Shamba ataachia Shoka liukate mti – Luka 3:9 “Na sasa hivi SHOKA limekwisha kuwekwa penye mashina ya MITI; basi kila usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa MOTONI”. Je! bado kuna dhambi iliyokung’ang’ania huwezi kuiacha? Mwambie Yesu atakupatia uwezo wa kushinda.

NAWATAKIA MAISHA MEMA YENYE KUZAA MATUNDA YA ROHO MTAKATIFU ILI TUWEZE KUISHI CHINI YA ULINZI WA MUNGU
Ev:  Eliezer Mwangosi.
0755808077 & 0652571733

CHANZO CHA LAANA DUNIANI

AMRI ZA MUNGU ZILIVYOBADIRISWA NA WANADAMU

AMRI KUMI ZA MUNGU
KAMA ZILIVYOANDIKWA NA MUNGU
KUTOKA 31:38, KUTOKA 20:3-17
1
Usiwe na Miungu mingine ila mimi
2
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, name nwarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika Amri zangu
3
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure
4
Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya Saba; kwa hiyo BWANA
akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
5
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
6
Usiue
7
Usizini
8
Usiibe
9
Usimshuhudie Jirani yako Uongo
10
Usitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.

AMRI ZA MUNGU KAMA ZILIVYOBADILISHWA NA WANADAMU
NA KUTIMIZA UNABII ULIOTABIRIWA
ISAYA 24:4-6,  DANIEL 7:25

1
Ndimi Bwana Mungu wako
Usiabudu miungu mingine

2
Usilitaje Bure Jina la Mungu

3
Shika kitakatifu siku ya Bwana

4
Waheshimu Baba na Mama

5
Usiue

6
Usizini

7
Usiibe

8
Usishuhudie Uongo

9
Usitamani mwanamke asiye mke wako

10
Usitamani mali ya Mtu Mwingine

SHERIA YA MUNGU YA UPENDO

AMRI KUMI ZA MUNGU - UPENDO
Kutoka 20:3-17

Mpende Bwana Mungu wako, Kwa moyo wako wote, na Kwa Roho yako yote, na akili zako zote. Mathayo 22:37

1
Usiwe na Miungu mingine ila mimi

2
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, name nwarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika Amri zangu

3
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure

4
Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya Saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.

Mpende Jirani yako kama nafsi yako.
Mathayo 22:39

5
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

6

Usiue

7

Usizini

8

Usiibe


9

Usimshuhudie jirani yako uongo

10

Usitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.

ZILIANDIKWA KWA CHANDA CHA MUNGU - KUTOKA 31:18

Tuesday, February 21, 2012

ITENGENEZENI NJIA YA BWANA

Neno la leo linatoka:  Matahayo 3:1-3
“Siku zile aliondoka Yohana mbatizaji akihubiri katika nyika ya uyahudi, na akisema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, sauti ya Mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni Mapito yake”

tAFAKARI:
Tangia kuumbwa ulimwengu, kanisa la Mungu limepitia historia inayojirudia, ya kumwacha Mungu na kugeukia hadithi za Uongo, ninaposema Kanisa nina maana kundi la watu wanaomwabudu Mungu. Siku zote Manabii na Mitume wa Uongo, kwa kutumia neno la Mungu vibaya na kwa  uwezo wa Roho bandia wamekuwa wakifanya Miujiza na Ishara nyingi kuwapoteza watu wa Mungu, na hatimaye watu wanatiwa Upofu na kutembea katika Giza la kiroho, yaani Dhambi inakuwa ni sehemu ya maisha.

Kama Yesu alivyotabiri, kizazi chetu kimefunikwa na Giza nene la Kiroho, wokovu Bandia unaendelea kushamiri, watu wanapenda mahubiri laini ya Mibaraka, Miujiza, Maombezi, kujazwa Roho, utajiri n.k. Lakini unashangaa kila kunapokucha ndio Uovu unazidi kati ya watu wa Mungu na Maisha ya Waumini bado yanazidi kuwa ya kukosa matumaini. Kabla ya kizazi hiki hakijaangamia, Mungu anatuma tena Ujumbe Mkali kupitia huduma ya NENO LA LEO, Ujumbe wa matengenezo, kama Nuhu alivyotumwa kuonya kabla ya gharika, na Lutu kabla ya Kuangamiza miji ya Zinaa, Sodoma na Gomora, na Kama Yohana mbatizaji alivyoiandaa njia ya Mwokozi.

Mwenye masikio na asikie, neno ambalo Roho ayaambia makanisa, Mfalme wa wafalme yuko mlangoni. Wakati shetani anakusanya watu wa Mungu chini ya falsafa ya Muungano wa makanisa wakiwa na mafundisho tofauti, huku wakiunda Dini moja na Selikali moja ya Dunia; Ujumbe wa mategenezo unahitajika kwa watu wa Mungu, kwani wengi watapotea bila kujua. Wewe mwenyewe ni Shahidi, wokovu wa siku hizi ni wa mdomoni, asilimia kubwa ni wa bandia – Hasira, chuki, ukali, ubinafsi, kujikweza, kupenda utajiri, visasi, upendeleo, uongo, masengenyo, uzinzi n.k. ni tabia zisizokoma kati ya waumini. Dini zimeingiza Ufisadi, Uasherati, Ushoga na usagaji, Pombe, Umizimu, kufuga majini ya kuleta utajili au ulinzi, hirizi na kuloga watu. WATUMISHI; Neno linasema Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni Mapito yake.    

TAHADHARI: Fuatilieni katika vyombo vya habari, viongozi wengi wa dini na waasisi wa makanisa hata ya Kiroho ni wafuasi (Member) wa Dini za mashetani, huku wanawatisha na Roho bandia, wakinena kwa Lugha, Miujiza, Ishara, Utabiri, Uponyaji n.k. Fuatilieni habari za Free Masons ili mjue mikakati yao ya kuunganisha Dini na Serikali za dunia. Wapendwa; Tunaishi nyakati za kufunga historia ya Dunia.

MUNGU AWABARIKI NA KUWALINDA, SIKU YA LEO IKAWE YA MAFANIKIO TELE

Ev:  Eliezer Mwangosi.
0755808077 & 0652571733
Kwa masomo zaidi fungua mitandao ifuatayo:   http://emwangosi.blogspot.com/ (VIJANA) http://kayanafamilia.blogspot.com/ (NDOA) http://matengenezo.blogspot.com/ (Ujumbe wa Matengenezo)

Saturday, February 18, 2012

ROHO ZA MANABII WA UONGO

NENO LA LEO:  Ufunuo 16:13-14
“Nikaona Roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule JOKA, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule NABII WA UONGO. Hizo ndizo Roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi”

TAFAKARI:
Nyakati tunazoishi ni za hatari sana kuliko nyakati zote ambazo Mwanadamu amewahi kuishi Duniani, Shetani anajua kuwa kiama yake pamoja na waovu aliowadanganya umekaribia. Ndio maana anafanya kila mbinu kuhakikisha anawateka wote hata waliodhamiria kuokolewa. Manabii wa Uongo ni Watumishi, Mitume, Wachungaji n.k. wanaohudumu madhabahuni, kwa Ishara na Miujiza mingi lakini wakiongozwa na Roho za Mashetani.

Tatizo kubwa linalowakumba wengi ni kutojua ni nani nabii wa Uongo? Make wote wanatumia Vitabu vya mwenyezi Mungu, wanatumia Jina la Yesu, wanajazwa Roho, wananena kwa Lugha n.k. Wapendwa Yesu alitoa tahadhari kuwa yote hayo watayafanya kwa Jina lake, lakini siku ya Mwisho atawambia “Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu” Mathayo 7:23. Wengi hawajui chanzo cha migawanyiko hii ya Dini na Madhehebu, wanafikiri ndio mafanikio ya kazi ya Mungu, lakini neno la Mungu lilitabili kuwa hiyo ni kazi ya Shetani.

Tusidanganyike, kila mmoja adhamirie kujifunza neno la Mungu na unabii wa siku za mwisho ili kujua siri za Shetani anazotumia kuwakusanya kwa ajili ya Jehanamu kwa kutumia Dini. Wewe jiulize inakuwaje Mungu awe kigeugeu? Mfano: Mungu gani aseme Pombe ni halali na sehemu nyingine aseme ni dhambi? au akataze Zinaa/Ushoga na sehemu nyingine aruhusu? wengine awaruhusu kufuga majini na wengine awaambie ni machukizo? au wengine watumie hirizi kuwa kinga na wengine awaambie ni dhambi? n.k.

TOFAUTI TUNAZOZIONA LEO KATIKA IMANI ZETU NI KAZI YA SHETANI ILIYOFANYIKA BAADA TU YA KULIHUJUMU KANISA LA MITUME WA YESU –  HERI NI KWAO WASOMAO NA KUSHIKA NENO LA KWELI LA MUNGU.

MUNGU WA UPENDO ATUPATIE SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE

Ev: Eliezer Mwangosi.