Saturday, February 18, 2012

ROHO ZA MANABII WA UONGO

NENO LA LEO:  Ufunuo 16:13-14
“Nikaona Roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule JOKA, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule NABII WA UONGO. Hizo ndizo Roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi”

TAFAKARI:
Nyakati tunazoishi ni za hatari sana kuliko nyakati zote ambazo Mwanadamu amewahi kuishi Duniani, Shetani anajua kuwa kiama yake pamoja na waovu aliowadanganya umekaribia. Ndio maana anafanya kila mbinu kuhakikisha anawateka wote hata waliodhamiria kuokolewa. Manabii wa Uongo ni Watumishi, Mitume, Wachungaji n.k. wanaohudumu madhabahuni, kwa Ishara na Miujiza mingi lakini wakiongozwa na Roho za Mashetani.

Tatizo kubwa linalowakumba wengi ni kutojua ni nani nabii wa Uongo? Make wote wanatumia Vitabu vya mwenyezi Mungu, wanatumia Jina la Yesu, wanajazwa Roho, wananena kwa Lugha n.k. Wapendwa Yesu alitoa tahadhari kuwa yote hayo watayafanya kwa Jina lake, lakini siku ya Mwisho atawambia “Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu” Mathayo 7:23. Wengi hawajui chanzo cha migawanyiko hii ya Dini na Madhehebu, wanafikiri ndio mafanikio ya kazi ya Mungu, lakini neno la Mungu lilitabili kuwa hiyo ni kazi ya Shetani.

Tusidanganyike, kila mmoja adhamirie kujifunza neno la Mungu na unabii wa siku za mwisho ili kujua siri za Shetani anazotumia kuwakusanya kwa ajili ya Jehanamu kwa kutumia Dini. Wewe jiulize inakuwaje Mungu awe kigeugeu? Mfano: Mungu gani aseme Pombe ni halali na sehemu nyingine aseme ni dhambi? au akataze Zinaa/Ushoga na sehemu nyingine aruhusu? wengine awaruhusu kufuga majini na wengine awaambie ni machukizo? au wengine watumie hirizi kuwa kinga na wengine awaambie ni dhambi? n.k.

TOFAUTI TUNAZOZIONA LEO KATIKA IMANI ZETU NI KAZI YA SHETANI ILIYOFANYIKA BAADA TU YA KULIHUJUMU KANISA LA MITUME WA YESU –  HERI NI KWAO WASOMAO NA KUSHIKA NENO LA KWELI LA MUNGU.

MUNGU WA UPENDO ATUPATIE SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE

Ev: Eliezer Mwangosi.

No comments:

Post a Comment