AMRI ZA MUNGU ZILIVYOBADIRISWA NA WANADAMU
AMRI KUMI ZA MUNGU KAMA ZILIVYOANDIKWA NA MUNGU KUTOKA 31:38, KUTOKA 20:3-17 1 Usiwe na Miungu mingine ila mimi 2 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, name nwarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika Amri zangu 3 Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure 4 Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya Saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa. 5 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako. 6 Usiue 7 Usizini 8 Usiibe 9 Usimshuhudie Jirani yako Uongo 10 Usitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako. | AMRI ZA MUNGU KAMA ZILIVYOBADILISHWA NA WANADAMU NA KUTIMIZA UNABII ULIOTABIRIWA ISAYA 24:4-6, DANIEL 7:25 1 Ndimi Bwana Mungu wako Usiabudu miungu mingine 2 Usilitaje Bure Jina la Mungu 3 Shika kitakatifu siku ya Bwana 4 Waheshimu Baba na Mama 5 Usiue 6 Usizini 7 Usiibe 8 Usishuhudie Uongo 9 Usitamani mwanamke asiye mke wako 10 Usitamani mali ya Mtu Mwingine |
No comments:
Post a Comment