Neno la leo linatoka: Matahayo 3:1-3
“Siku zile aliondoka Yohana mbatizaji akihubiri katika nyika ya uyahudi, na akisema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, sauti ya Mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni Mapito yake”
tAFAKARI:
Tangia kuumbwa ulimwengu, kanisa la Mungu limepitia historia inayojirudia, ya kumwacha Mungu na kugeukia hadithi za Uongo, ninaposema Kanisa nina maana kundi la watu wanaomwabudu Mungu. Siku zote Manabii na Mitume wa Uongo, kwa kutumia neno la Mungu vibaya na kwa uwezo wa Roho bandia wamekuwa wakifanya Miujiza na Ishara nyingi kuwapoteza watu wa Mungu, na hatimaye watu wanatiwa Upofu na kutembea katika Giza la kiroho, yaani Dhambi inakuwa ni sehemu ya maisha.
Kama Yesu alivyotabiri, kizazi chetu kimefunikwa na Giza nene la Kiroho, wokovu Bandia unaendelea kushamiri, watu wanapenda mahubiri laini ya Mibaraka, Miujiza, Maombezi, kujazwa Roho, utajiri n.k. Lakini unashangaa kila kunapokucha ndio Uovu unazidi kati ya watu wa Mungu na Maisha ya Waumini bado yanazidi kuwa ya kukosa matumaini. Kabla ya kizazi hiki hakijaangamia, Mungu anatuma tena Ujumbe Mkali kupitia huduma ya NENO LA LEO, Ujumbe wa matengenezo, kama Nuhu alivyotumwa kuonya kabla ya gharika, na Lutu kabla ya Kuangamiza miji ya Zinaa, Sodoma na Gomora, na Kama Yohana mbatizaji alivyoiandaa njia ya Mwokozi.
Mwenye masikio na asikie, neno ambalo Roho ayaambia makanisa, Mfalme wa wafalme yuko mlangoni. Wakati shetani anakusanya watu wa Mungu chini ya falsafa ya Muungano wa makanisa wakiwa na mafundisho tofauti, huku wakiunda Dini moja na Selikali moja ya Dunia; Ujumbe wa mategenezo unahitajika kwa watu wa Mungu, kwani wengi watapotea bila kujua. Wewe mwenyewe ni Shahidi, wokovu wa siku hizi ni wa mdomoni, asilimia kubwa ni wa bandia – Hasira, chuki, ukali, ubinafsi, kujikweza, kupenda utajiri, visasi, upendeleo, uongo, masengenyo, uzinzi n.k. ni tabia zisizokoma kati ya waumini. Dini zimeingiza Ufisadi, Uasherati, Ushoga na usagaji, Pombe, Umizimu, kufuga majini ya kuleta utajili au ulinzi, hirizi na kuloga watu. WATUMISHI; Neno linasema Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni Mapito yake.
TAHADHARI: Fuatilieni katika vyombo vya habari, viongozi wengi wa dini na waasisi wa makanisa hata ya Kiroho ni wafuasi (Member) wa Dini za mashetani, huku wanawatisha na Roho bandia, wakinena kwa Lugha, Miujiza, Ishara, Utabiri, Uponyaji n.k. Fuatilieni habari za Free Masons ili mjue mikakati yao ya kuunganisha Dini na Serikali za dunia. Wapendwa; Tunaishi nyakati za kufunga historia ya Dunia.
MUNGU AWABARIKI NA KUWALINDA, SIKU YA LEO IKAWE YA MAFANIKIO TELE
Ev: Eliezer Mwangosi.
0755808077 & 0652571733
Kwa masomo zaidi fungua mitandao ifuatayo: http://emwangosi.blogspot.com/ (VIJANA) http://kayanafamilia.blogspot.com/ (NDOA) http://matengenezo.blogspot.com/ (Ujumbe wa Matengenezo)
Amina
ReplyDelete