NENO LA LEO: Yeremia 25:34-35
Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuwawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa. Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka.
TAFAKARI:
Wapendwa! Tunapaswa kujua kuwa tunaishi nyakati za Mwisho na hatari, Yesu alitabiri kuwa wengi hawataokolewa si kwa sababu waliamua hivyo, laa, bali kwa sababu walikoseshwa na viongozi wao wa Dini. Tunashuhudia kila kukicha Wachungaji, Manabii na Mitume wanajitokeza na kuanzisha makanisa, na ujumbe mkubwa ni BARAKA, UTAJIRI, UPONYAJI NA MIUJIZA MINGI. Wachungaji wengi leo ni wachungaji wa MSHAHARA, makanisa ni vitega uchumi sawa na machimbo ya Madini, ndio maana hawana ujasiri wa kukemea uovu. Na wengine bila aibu wanakula Kondoo zao.
Tunashuhudia Wachungaji wengi wakijihusisha na mambo ya aibu kwa SIRI na wengine hata kuanikwa na vyombo vya habari. Pia wengi leo ni wafuasi wa dini za waabudu mashetani na wengine ni free mason, kwa hila wanalaghai watu wengi kwa kujazwa ROHO bandia na Miujiza Mingi – Yesu alisema “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, HATA WALIO WATEULE. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Mathayo 24:24-25, Mathayo 7:21-23.
Wengi wataangamia kwa kukosa MAARIFA (Hosea 4:6), Wapendwa! Miujiza, Kujazwa Roho,Upako, Kunena kwa Lugha n.k. Sio kithibitisho pekee cha Kumtambua mtumishi wa Mungu, kwani SHETANI pia anafanya hayo kwa hila, tunapaswa kujiepusha naye. Siku nyingine nitatoa somo la jinsi ya kuwatambua watumishi wa Mungu na Bandia.
MUNGU WA AMANI AWALINDE NA KUWAPATIA SIKU NJEMA
Ev: Eliezer Mwangosi
0755808077 & 0652571733
Kwa masomo zaidi fungua mitandao ifuatayo: http://emwangosi.blogspot.com/ (VIJANA) http://kayanafamilia.blogspot.com/ (NDOA) http://matengenezo.blogspot.com/ (UKWELI HALISI)
No comments:
Post a Comment