AMRI KUMI ZA MUNGU - UPENDO
Kutoka 20:3-17
Mpende Bwana
Mungu wako, Kwa moyo wako wote, na Kwa Roho yako yote, na akili zako zote.
Mathayo 22:37
[Upendo kati ya Mwanadamu na Mungu]
1
Usiwe na Miungu mingine ila mimi
2
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote
kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini
ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni
Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu
na cha nne cha wanichukiao, name nwarehemu maelfu elfu wanipendao, na
kuzishika Amri zangu
3
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana Bwana
hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure
4
Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende
mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku
hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala
mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye
ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi,
na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya Saba; kwa hiyo BWANA
akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
|
Mpende Jirani
yako kama nafsi yako.
Mathayo 22:39
[Upendo kati ya Mwanadamu na Mwenzie]
5
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi
katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
6
Usiue
7
Usizini
8
Usiibe
9
Usimshuhudie jirani yako uongo
10
Usitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako,
wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala
chochote alicho nacho jirani yako.
|
ZILIANDIKWA
KWA CHANDA CHA MUNGU - KUTOKA
31:18
No comments:
Post a Comment